WANAFUNZI WA KOZI YA “AGRICULTURE INVESTMENT AND BANKING” WASHIRIKI MAONESHO YA 18 YA WIKI YA KUMBUKIZI YA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE

Wanafunzi wa mwaka wa pili na wa tatu wanaochukua kozi ya Uwekezaji katika Kilimo na Benki inayotolewa na Chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) chini ya ndaki ya uchumi na stadi za biashara (CoEBS) katika idara ya usimamizi wa biashara (DBM) wamepata wasaa wa kushiriki maonesho haya ya kumbukizi ya hayati Edward Moringe Sokoine.

Wanafunzi hao chini ya kampuni yao ifahamikayo kwa jina la REE FARM INVESTMENT inaendesha shughuli za kiuchumi na kijamii mkoani Morogoro kupitia programu mahususi ijulikanayo kama “JAMII KILIMO”.


Wanafunzi hao wanatoa huduma mbalimbali kama vile mafunzo ya uwekezaji na utunzaji wa mimea kwa vitendo, ushauri katika uwekezaji hasa wa kilimo, mashamba darasa pamoja na kutoa muongozo wa upatikanaji wa pembejeo bora za kilimo.

Maonesho hayo yamehudhuriwa na wadau mbalimbali ndani na nje ya Chuo Kikuu cha cha Sokoine cha Kilimo ambayo yamekuwa yakifanyika kila siku kuanzia tarehe 23/5/2023 hadi 26/5/2023.

 

 

Katika picha ni matukio mbalimbali wanafunzi hao wamekuwa wakiyafanya katika maonesho hayo.

Related Posts